Watu 130 wameambukizwa virusi vya corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita baada ya sampuli 4,918 kupimwa na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 100,323.
Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema kuwa watu 66 wamepona kutokana na virusi hivyo na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 83,691.
Mtu mmoja amefariki kutokana na ugonjwa huo na kufikisha idadi ya maafa kuwa 1,751.
Wagonjwa 489 wamelazwa katika hospitali mbalimbali 28 wakilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Msambao wa visa hivi ni kama ifuatavyo: Nairobi 66,Taita Taveta 18, Mombasa 9, Nakuru na Narok 6, Siaya, Uasin Gishu na Kiambu 4, Kilifi 2,Kisumu, Bungoma, Busia, Kajiado, Kakamega, Nyamira na Nyandarua 1.