DCI wamshika mshukiwa wa mauaji ya mpenziwe Njiru, alitaka kujiua

0

Hatimaye makachero wa idara ya upelelezi nchini DCI wamemshika jamaa anayedaiwa kumuua aliyekuwa mpenziwe kwa kumfunga mikono na kisha kumchoma katika eneo la Njiru jijini Nairobi.

Mshukiwa huyo alikuwa anatishia kujiua kwa kujirusha kutoka juu ya roshani ila makachero wa DCI wamefaulu kumshawishi asijitoe uhai na hivyo kumkamata.

Mshukiwa amekuwa mafichoni kuanzia Ijumaa iliyopita anapodaiwa kutekeleza unyama huyo na alikuwa amejifungia katika chumba kimoja mtaani Kayole.

Wafanyikazi wa nyumbani wa marehemu katika taarifa yao kwa Polisi walieleza kuwa mwajiri wao aliwapa pumziko la muda kuanzia mwendo wa saa mbili asubuhi kwa sababu yeye na mpenzi wake walitaka kujaribu kutatua tofauti zilizokuwa baina yao.

Hata hivyo baadaye jioni nyumba yao ilionekana ikiteketea na juhudi za kujaribu kuzima moto huo wala kumuokoa ziliambulia patupu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here