Rais Uhuru Kenyatta amezindua miradi ya maendeleo katika kaunti ya Mombasa anapolenga kuhakikisha kuwa maendeleo yamefika mashinani.
Akiwa ameandamana na gavana wa Mombasa Hassan Joho, rais Kenyatta amezindua ujenzi wa kivukio cha Makupa kinachogharimu Sh4.5b.
Ujenzi wa kivukio hicho unatazamiwa kukamilisha Januari mwaka 2022 na kurahisisha usafiri wa majini katika kaunti ya Mombasa.
Gavana wa Joho amesema hatua hiyo itatoa afueni kwa wakaazi ambao wamekuwa wakihangaika wanaposafiri.
Rais Kenyatta ametumia fursa hiyo kuwarai Wakenya kuunga marekebisho ya kataba kupitia mchakato wa BBI.
Kiongozi wa taifa vile vile ameongoza ujenzi wa daraja la Liwatoni kitakachounganisha kisiwa cha Mombasa na Ras Bofu kilichoko Likoni.
Daraja hilo la wasafiri wa miguu ambalo limeninginia juu ya bahari limegharimu serikali shilingi billion 1.9 na litasaidia kupunguza msongamano wa watu kwa feri na usafiri wa makontena kutoka Mombasa.









