Mahakama kuu imewaagiza wabunge kuwarudishia Wakenya Sh3b walizojilipa kama marupurupu kinyume cha sheria miaka miwili iliyopita.
Jopo la majaji watatu Weldon Korir, Pauline Nyamweya na John Mativo limemuagiza karani wa bunge la Senate na lile la kitaifa kurejesha pesa hizo kwa kukata kwenye mishahara na marupurupu ya wabunge.
Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na tume ya kuratibu mishahara ya watumishi wa umma SRC pamoja na mwanaharakati Okiya Omtatah ambao walipinga marupurupu ya Sh250,000 kwa wabunge wote 416.
Hii inamaanisha kuwa kila mbunge atahitajika kulipa Sh7.2M katika muda wa mwaka mmoja ujao.