IEBC yapokea sahihi za BBI

0

Hatimaye saini za BBI zilizokusanywa wiki iliyopita zimewasilishwa kwa tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kwa ukaguzi.

Mwenyekiti wa kamati ya BBI iliyosimamia shughuli hiyo ya kukusanya sahihi hizo Dennis Waweru amemkabidhi mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati saini hizo zaidi ya million nne katika hafla afisi za tume hiyo jijini Nairobi.

Chebukati anasema wataanza kuzikagua saini hizo baada ya kupokea pesa kutoka kwa wizara ya fedha.

Mwenyekiti mwenza aliyepia mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohammed amesema hawajabadilisha lolote katika mswada ambao wamewasilisha kwa tume hiyo.

Nao viongozi wanaosukuma ajenda ya BBI wakiongozwa na mbunge wa Makadara George Aladwa wameelezea matumaini yao kwamba tume ya uchaguzi IEBC itakamilisha kibarua cha kukagua na kuidhinisha sahihi za BBI ili kuharakisha mchakato wa kufanyia katiba marekebisho.

Baada ya ukaguzi huo, mswada huo utatumwa kwa mabunge ya kaunti iwapo saini zitakoidhinishwa zitakuwa zaidi ya million moja.

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here