Watu 1,060 wapona ugonjwa wa corona Kenya kwa siku moja

0

Watu 1,060 wamepona ugonjwa wa corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi hiyo kuwa 71,254.

Maambukizi ya ugonjwa huo yanaendelea kuongezeka huku waziri wa afya Mutahi Kagwe akitangaza kuwa watu 644 zaidi wameambukizwa virusi hivyo baada ya kupima sampuli 6,811 na hivyo kuwa 90,305.

Wagonjwa wengine 16 wamefariki kutokana na makali ya ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliofariki kuwa 1,568.

Wakati uo huo wagonjwa wengine 994 wamelazwa katika hospitali mbalimbali, 7,844 wakihudumiwa nyumbani.

Wagonjwa 55 wamelazwa katika chumba cha watu mahututi ICU, 27 wakisaidiwa na mashine kupumua.

Kaunti ya Nairobi inaendelea kuongoza kwa kuandikisha visa 158, Kisumu 69, Mombasa  67, Murang’a  56, Taita Taveta 36, Nakuru 31, Meru 26, Bungoma na Laikipia 19.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here