Uhuru awapongeza Wakenya kwa kulipa ushuru, akutana na Pope Francis

0

Rais Uhuru Kenyatta amewashukuru Wakenya kwa kulipa ushuru kwa wakati na hivyo kulisaidia taifa kutekeleza majukumu yake kifedha kipindi hiki kigumu cha corona.

Akihutubu kupitia njia ya video kuadhimisha siku ya mlipa ushuru, rais Kenyatta vile vile ameipongeza mamlaka ya kukusanya ushuru (KRA) kwa kujikakamua kukusanya pesa licha ya hali ngumu ya kiuchumi inayosababishwa na COVID19.

Hayo yakijiri, rais Uhuru Kenyatta ameanza rasmi ziara yake jijini Vatican, Italia kwa kufanya mazungumzo na kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Pope Francis.

Mazungumzo hayo yaliangazia elimu, afya ikizingatiwa kwamba kanisa katoliki linafadhili shule pamoja na vituo mbalimbali vya afya, usalama na amani katika kanda hii.

Rais Kenyatta hapo kesho Jumamosi ameratibiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Sergio Materrela kuangazia maswala yanayohusu ushirikiano baina ya mataifa haya mawili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here