Wanachama wa BBI wajibizana hadharani kuhusu ripoti ya kamati hiyo

0

Katibu mwenza wa kamati ya BBI wakili Paul Mwangi ametaja kama porojo madai kwamba walihadaiwa kukubali ripoti ya mwisho ya BBI iliyoongezwa mambo ambayo hawajui.

Meja mstaafu John Seii mmoja wa wanachama wa kamati hiyo alidai kwamba baadhi ya mambo ambayo hakuwa wamejadiliana kuyahusu ikiwemo kubuniwa kwa wadhifa wa waziri mkuu na manaibu wake wawili pamoja na kuongeza kwa idadi ya maeneo bunge hayakuwa miongoni mwa mambo walikuwa wamekubaliana yawe kwenye ripoti ya mwisho.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, wakili Mwangi amesema anashangaa ni vipi meja ambaye ni mtu na heshima zake anawadanganya Wakenya mchana peupe ihali tangu mwaka 2018 amekuwa chini ya shinikizo wakati maoni ya umma yalikuwa yanakusanywa.

Mwangi amefichua kuwa zaidi ya mara moja, Seii alikutwa akipiga picha kisiri mikutano ya jopo hilo na alipoulizwa alidai kuwa alikuwa haoni vizuri kwa sababu alikuwa na matatizo ya macho. Hili liliwalazimu wanachama wa kamati hiyo kumkanya dhidi ya tabia hiyo na wanashangaa alivyoibuka na madai kuwa walilaghaiwa kutia saini ripoti ya mwisho.

Ameongeza kuwa maswala yote ambayo mwenzao anadai hayakuwa kwenye ripoti hiyo yalikuwepo tokea mwanzo ikiwemo wadhifa wa waziri na kuongezwa kwa idadi ya maeneo bunge.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here