Idadi ya maambukizi ya virusi vya corona nchini imeongezeka na kufikia 60,704 baada ya watu 1,104 kupatikana na ugonjwa kati ya sampuli 7,153 zilizopimwa katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.
Waliopona wamefikia 40,131 baada ya wagonjwa wengine 938 kupona huku maafa yakifikia 1,093 baada ya watu wengine 21 zaidi kufariki.
Wagonjwa 1,300 wamelazwa katika hospitali mbalimbali nchini, 60 wakiwa katika chumba wagonjwa watu mahututi ICU.
Nairobi imeandikisha visa 347, Mombasa 198, Nakuru 73, Uasin Gishu 69, Meru 63, Kiambu 40 na Kisumu 36.