Uhaba wa fedha wawakodolea macho walimu wakuu shule zikifunguliwa

0

Shughuli ya wanafunzi kote nchini kurejea shuleni imeanza rasmi hii leo Jumatatu, tarehe 27 Mei 2026, shule zikifunguliwa kwa muhula wa pili ambao ni mrefu zaidi katika kalenda ya masomo, ukitarajiwa kudumu kwa wiki 14 hadi Julai 31, 2026.

Shule zinafunguliwa huku kukiwa na changamoto kadhaa, ikiwemo kucheleweshwa kwa mgao wa fedha za elimu na upungufu wa fedha hizo.

Mwenyekiti wa Muungano wa Walimu Wakuu wa Shule za Sekondari, Willy Kuria, amesema shule nyingi zinaendelea kukabiliwa na hali ngumu ya kifedha.

Wanafunzi wa shule za sekondari wanatengewa shilingi 22,000 kwa mwaka, wale wa Junior Secondary School (JSS) shilingi 15,000, na shule za msingi shilingi 1,400.

Hata hivyo, serikali haijakuwa ikitoa fedha hizo kikamilifu, hali ambayo Katibu katika Wizara ya Elimu, Julius Bitok, amesema inachangiwa na ongezeko la idadi ya wanafunzi na changamoto za bajeti.

Aidha, wabunge wameitaka Wizara ya Elimu kukiri kuwa serikali haiwezi kufadhili elimu kikamilifu.

Wakati uohuo, kuna malalamishi mapya kutoka kwa walimu kuhusu bima ya afya ya jamii SHA, wakisema haijawa na manufaa sawa na ile ya awali ya MINNET, huku wakitoa makataa ya siku 14 kwa serikali kuboresha bima hiyo, la sivyo wagome.

“Baadhi ya hospitali zinakataa SHA au zinahitaji malipo ya fedha taslimu kabla ya kutoa huduma. Manufaa ya SHA si ya kina kama ilivyokuwa kwenye mpango wa awali wa MINNET.” Walimu wamesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here