Mvua kubwa inatarajiwa kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini kati ya Jumanne, Juni 30 na Julai tarehe Sita huku vipindi vya baridi na mawingu vikiendelea kushuhudiwa katikamaeneo mbalimbali.
Kulingana na Idara ya Utabiri wa Hali ya anga mvua inatarajiwa katika bonde la ziwa Viktoria, Nyanda za Juu Mashariki na Magharibi ya bonde la Ufa, Bonde la ufa Pamoja na Ukanda wa pwani.
Kaunti zinazotarajiwa kupokea mvua ya kati ya Milimita 5 na 10 katika siku 7 zijazo ni Pamoja na Narok, Nyeri, Nakuru, Kakamega, Bungoma, Transnzoia, Kwale, Kilifi, Lamu Pamoja na Tana River.
Wakati uo huo ripoti ya Pamoja ya shirika la chakula na kilimo duniani FAO Pamoja na shirika la mpango wa chakula duniani WFP imeonya kuwa Kenya ni miongoni mwa mataifa 22 yanayaoweza kuathirika pakubwa na mvua ya El nino inayotarajiwa kuanza kunyesha kati ya mwishoni mwa mwaka 2026 na mapema mwaka 2027.
“Kenya ni miongoni mwa mataifa 22 yanyaoweza kuathirika na Mvua ya El Niño, na kutishia usalama wa chakula na kilimo katika maeneo mengi hadi mwaka wa 2027” ripoti hiyo imesema.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa Elnino inaweza kusababisha mvua kubwa kuliko kawaida, mafuriko, uharibifu wa mazao na miundombinu ya kilimo.
“Kwa upande mwingine, kati ya Oktoba na Desemba, katika maeneo yenye misimu miwili ya mvua ya Pembe ya Afrika, ikiwa ni pamoja na Somalia, Kenya, Uganda na mashariki mwa Ethiopia, El Niño inahusishwa na hatari kubwa ya mvua na mafuriko yanayozidi wastani,” ripoti hiyo inasema.









