Utafiti wa Infotrak Waibua vongozi Waliobobea Kwenye Utendakazi wao Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2027.

0

Seneta wa Kaunti ya Kirinyaga Kamau Murango, Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino na Mwakilishi wa Kike wa kaunti ya Kirinyaga Jane Maina wameibuka kama viongozi wanaofanya vyema zaidi nchini.

Haya yamebainika katika utafiti wa Infotrak, uliowahusisha zaidi ya wananchi 87,000 kutoka kaunti zote 47, ukilenga kutathmini utendaji wa viongozi waliochaguliwa kwa misingi ya mtazamo wa wananchi.

Utafiti huo uliotolewa na Shirika la Infotrak, uliwapima Wabunge kwa kuzingatia mtazamo wa wananchi kuhusu utendakazi wao, uwakilishi, uwazi, na utekelezaji wa miradi katika maeneobunge yao.

“Uchaguzi huwapa wakenya mamlaka ya kuchagua viongozi. Wakenya wanaendelea kuchunguza, kutathmini na kuangazia ubora wa uongozi wanaopokea.” Infotrak ilibainisha.

Kulingana na Infotrak Seneta wa Kaunti ya Kirinyaga Kamau Murango ametajwa kuwa Seneta bora zaidi nchini kufuatia utendakazi wake akiongoza kwa asilimia 69, akifuatwa kwa ukaribu na Seneta wa Nyandarua John Methu kwa asilimia 68, kisha Joe Nyutu wa Murang’a akishika nafasi ya tatu kwa asilimia 65.

Seneta wa Nandi Samson Cherargei anashikilia nafasi ya nne kwa asilimia 64, akifuatwa na Aaron Cheruiyot wa Kericho mwenye asilimia 63, wakikamilisha tano bora.

Wengine waliotajwa ni Seneta wa Baringo Vincent Kiprono na wa Kisii Richard Onyonka wote wakiwa na asilimia 62, pamoja na Seneta wa Makueni Dan Maanzo.

Aidha, Edwin Sifuna wa Nairobi na Steve Lelelgwe wa Samburu kila mmoja akiwa na asilimia 61, wakifunga orodha ya maseneta 10 bora nchini.

Maseneta wengine waliojitokeza katika orodha hiyo ni pamoja na Ali Roba wa Mandera, Enoch Wambua wa Kitui, Julius Murgor Pokot Magharibi, Hillary Sigei wa Bomet na Jackson Mandago wa Uasin Gishu, ambao viwango vyao vilikuwa kati ya asilimia 58 na 60.

Kwa upande wa Wawakilishi wa wanawake Jane Maina wa Kaunti ya Kirinyaga ameongoza kwa mara ya pili sasa kwa kupata asilimia 67 akifuatwa na Rael Kasiwai wa Pokot Magharibi kwa asilimia 61, huku Pauline Lenguris wa Samburu na Elsie Muhanda wa Kakamega wakilingana kwa asilimia 60.

Rose Mumo wa Makueni alipata asilimia 58, akifuatiwa na Cecilia Ngitit wa Turkana kwa asilimia 56, Cynthia Muge wa Nandi kwa asilimia 55, Bensuda Osogo wa Homa Bay kwa asilimia 54.

Irene Kasalu wa Kitui pamoja na Susan Nduyo wa Tharaka Nithi, walipata asilimia 53.

Kwa upande wa Wabunge, Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino ameibuka Mbunge bora zaidi katika utafiti huo kwa mara ya pili sasa, akipata asilimia 80 ya uidhinishaji wa utendakazi wake akifuatwa na Mbunge wa Kabuchai Joseph Kalasinga akishika nafasi ya pili kwa asilimia 78.

Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro na Mbunge wa Taveta John Bwire wamefunga nafasi ya tatu kwa asilimia 76 kila mmoja.

Mbunge wa Samburu Magharibi Josephine Naisula Lesuuda, Kimilili Didmus Barasa, Mogotio Reuben Kiborek, Keiyo Kusini Gideon Kimaiyo, Belgut Nelson Koech na Mbunge wa Mukureiwini Gichohi Kaguchia wakipata asilimia 73 kila mmoja.

Wengine walioingia katika orodha ya wabunge bora ni Mbunge wa Aldai Marianne Kitany, Peter Salasya (Mumias Mashariki), Jackson Lekumontare (Samburu Mashariki), Danson Mwashako(Wundanyi), Erastus Kivasu Nzioka(Mbooni), Omar Mwinyi(Changamwe) na Walter Owino wa Awendo, wote wakiwa na alama kati ya asilimia 70 hadi 72.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here