Baraza la Mawaziri limeagiza kufanyika kwa uchunguzi wa kina kuhusu madai ya wizi wa misharara serikalini baada ya ukaguzi kubaini dosari zinazoshukiwa kuigharimu serikali takriban Shilingi bilioni 6.2 katika idara 12 za serikali.
Haya yanajiri kufuatia ukaguzi uliobainisha fedha ambazo hazijaidhinishwa kwenye Rekodi za mishahara, malipo yasiyo halali, udhaifu katika usimamizi wa makato na mapungufu makubwa ya usimamizi wa mifumo ya mishahara.
“Uamuzi huo umeafikiwa baada ya ukaguzi wa kina wa mfumo wa mishahara serikalini kubaini udhaifu mkubwa katika usimamizi wa mishahara. Ukaguzi wa sampuli katika idara 12 kati ya 53 za serikali uligundua dosari zinazoshukiwa kugharimu serikali takriban shilingi bilioni 6.2.”
“Dosari hizo ni pamoja na mabadiliko yasiyoidhinishwa kwenye rekodi za mishahara, malipo yasiyo halali, udhaifu katika usimamizi wa makato ya kisheria, pamoja na mapungufu makubwa katika usimamizi wa mfumo wa mishahara.” Taarifa hiyo ya Baraza la Mawaziri imesema.
Kutokana na hilo Baraza la Mawaziri limeiagiza Idara ya upelelezi na makosa ya jinai DCI kuchunguza madai hayo, kudhibitisha idadi ya wafanyikazi zinazotumika katika mfumo wa mishahara kuvunja mitandao ya wahalifu wanaodaiwa kuuhujumu mfumo huo na kuhakikisha kuwa fedha za umma zilizopotea zinarejeshwa.
Aidha serikali imeagiza kufanyika kwa ukaguzi wa mifumo ya mishahara katika Idara zote za serikali na taasisi za umma Pamoja na kuhamisha wizara, Idara na mashirika yote ya serikali kwenye mfumo mpya wa usimamizi wa wafanyikazi na mishahara.
Wakati uo huo Baraza la Mawaziri limeidhinisha sera ya kitaifa ya huduma za uhamishaji wa kazi kwa njia ya kidijitali BPO ili kuifanya Kenya Kuwa Kitovu cha Kimataifa cha Huduma hizo na kubuni ajira kwa vijana.
Ili kujiandaa kwa mvua ya El Nino inayotarajiwa baadaye mwaka huu Baraza hilo limebuni Kamati maalum ya maandalizi na kukabili El Nino nchini chini ya Uenyekiti wa Naibu wa Rais Professa Kithure Kindiki.
“Mvua ya El Niño inaendelea kujitokeza, na mamilioni ya watu wanaokabiliwa na uhaba wa chakula wako katika hatari.” Taarifa imeongeza.
“Mvua hii ya El Niño inatarajiwa kuleta ukame kusini mwa Afrika, Amerika ya Kati, sehemu za Asia na Pasifiki, huku ikiongeza hatari ya mafuriko na dhoruba katika Pembe ya Afrika na baadhi ya maeneo ya Asia.” Imeeleza.
Haya yanajiri baada ya ripoti ya Pamoja ya shirika la chakula na kilimo duniani FAO Pamoja na shirika la mpango wa chakula duniani WFP kuonya kuwa Kenya ni miongoni mwa mataifa 22 yanayaoweza kuathirika pakubwa na mvua ya El nino inayotarajiwa kuanza kunyesha kati ya mwishoni mwa mwaka 2026 na mapema mwaka 2027.
“Kenya ni miongoni mwa mataifa 22 yanyaoweza kuathirika na Mvua ya El Niño, na kutishia usalama wa chakula na kilimo katika maeneo mengi hadi mwaka wa 2027” ripoti hiyo imesema.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa El Niño inaweza kusababisha mvua kubwa kuliko kawaida, mafuriko, uharibifu wa mazao na miundombinu ya kilimo.
“Kwa upande mwingine, kati ya Oktoba na Desemba, katika maeneo yenye misimu miwili ya mvua ya Pembe ya Afrika, ikiwa ni pamoja na Somalia, Kenya, Uganda na mashariki mwa Ethiopia, El Niño inahusishwa na hatari kubwa ya mvua na mafuriko yanayozidi wastani,” ripoti hiyo inasema.
Aidha Serikali imeidhinisha miradi kadhaa ya maendeleo ukiwemo mradi wa kuboresha utendaka kazi wa mahakama wenye dhamani ya shilingi bilioni 26 kwa ushirikiano na Benki Kuu ya Dunia Pamoja na fedha za ziada za shilingi bilioni 16.6 kukamilisha mradi wa Bwawa la Mwache katika kaunti ya Kwale.









