Rais Atia Saini Kuwa Sheria Mswada wa Marekebisho ya Benki Kuu.

0

Rais William Ruto ametia Saini kuwa sheria miswada miwili inayolenga kuimarisha sekta ya fedha nchini na kufanya marekebisho ya mfumo wa malipo ya kustaafu ya wabunge kuendana na Katiba na sheria ya sasa.

Miswada iliyopitishwa inajumuisha marekebisho ya sheria ya benki kuu CBK na sheria ya marekebisho ya malipo ya kustaafu ya wabunge katika hafla iliyofanyika kwenye Ikulu ya Nairobi.

Kupitia sheria hiyo mpya CBK itaendelea kuwa na mamlaka ya kutoa msaada wa kifedha wa dharura kwa taasisi za kifedha zinazokumbwa na matatizo ya muda kama vile kuamua taasisi zitakazonufaika, viwango vya riba na muda wa msaada huo.

Sheria hiyo pia inaruhusu msaada huo kutolewa kwa kipindi cha hadi miezi 12 na katika mazingira maalum kuongezwa hadi miaka 5 kulingana na hali ya taasisi husika.

Wakati uo huo Rais ameidhinisha marekebisho ya sheria ya pensheni ya wabunge ambayo yalipendekezwa na mbunge wa Kitui ya Kati Makali Mulu.

Mswada huo wa mwaka 2023, unawapa Maseneta na Wabunge haki sawa za pensheni kulingana na Katiba ya mwaka 2010.

Sheria hiyo pia imeongeza umri wa mtoto anayestahili kunufaika na pensheni kutoka miaka 16 hadi 18, huku malipo ya gratuity yakibaki kutolewa kwa wabunge watakaohudumu kwa kipindi kisichozidi miaka mitano.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here