Waliangua vilio kilio, machozi ya huzuni yakimtiririka kila mmoja wao wakati wanafunzi wa shule ya wasichana ya Oyugi Ogango katika eneo la Rongo kaunti ya Migori walifahamishwa kwamba mwalimu wao mkuu amefariki.
Wanafunzi hao wa kidato cha nne walikosa wa kuwafariji walipopewa taarifa hizo za kufariki kwa mwalimu wao Martha Ouma alipatwa na matatizo ya kupumua kabla ya kukata roho.
Hata hivyo maafisa wa muungano wa walimu KUPPET kaunti ya Migori wamekanusha kwamba kifo chake kimesababishwa na corona.
Waziri wa elimu katika kaunti hiyo Iscar Oluoch amesema chanzo cha kifo hicho bado hakijabainika.
Walimu wengine watano wako kwenye karantini kwa mujibu wa muungano huo.
Wakati uo huo
Wanafunzi 38 wa shule ya upili ya Marafa kaunti ya Kilifi wamekutwa na virusi vya corona.
Gavana wa kaunti hiyo Amason Kingi anasema wanafunzi hao wamewekwa karantini wakiendelea kupokea matibabu huku akisema kuwa kaunti hiyo imeanza kushuhudia idadi ya juu ya maambukizi.









