Watu 15 zaidi wafariki kutokana na corona, maafa yakifikia 1,302

0

Idadi ya visa vya corona nchini imefikia 71,729 baada ya watu 925 kupatikana na ugonjwa huo kati ya sampuli 5,559 zilizopimwa katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe anasema idadi ya maafa imeongezeka na kufikia 1,302 baada ya watu 15 zaidi kufariki.

Idadi ya waliopona imeongezeka na kufikia 47,262 baada ya watu wengine 1,018 kupona ugonjwa huo.

Nairobi imerokodi visa 358, Kiambu 102, Mombasa 59, Nakuru & Nyeri 39 na Machakos 32.

Kufikia leo, wagonjwa 1,237 wangali wamelazwa katika hospitali mbalimbali huku 6,257 wakishughulikiwa nyumbani.

Wagonjwa walio katika chumba cha watu hali mahututi (ICU) ni 62 huku 26 wakisaidiwa na mashine kupumua.

Wakati uo huo

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema wahudumu wa afya waliofariki kutokana na ugonjwa wa corona imeongezeka na kufikia 30 huku walioambukizwa virusi hivyo wakiwa 2,352.

Kati ya hao waliokutwa na ugonjwa huo ni wanaume 1,177 na wanawake 1,175.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here