Ruto ataka NHIF igharamie matibabu ya corona

0

Naibu rais William Ruto anaitaka bima ya matibabu NHIF kugharamia matibabu ya corona kwa wanachama wake.

Ruto haswaa amewalenga wanafunzi wanaorejea shuleni Januari mwaka ujao akisema hili litafaulu iwapo NHIF itawezeshwa kuafikia lengo hilo.

Akifika mbele ya bunge la Senate, waziri wa afya Mutahi Kagwe alifutilia mbali uwezekano wa NHIF kugharamia matibabu ya wagonjwa wa corona kwa sababu gharama hiyo ni ya juu mno na ni janga ambalo halikutarajiwa.

Wito wa naibu rais unawadia siku moja baada ya tume ya huduma za walimu TSC kutangaza kuwa walimu watagharamiwa matibabu ya ugonjwa huo wa COVID19 baada ya kukutana na wadau husika.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here