Serikali imetoa hakikisho kwamba imeweka mikakati makhususi kuhakikisha kwamba mitihani ya kitaifa inaendelea kote nchini pasipo kutatizika.
Msemaji wa serikali kanali mstaafu Cyrus Oguna amesema kila kitu kii shwari kabla ya kuanza kwa mitihani hiyo ikiwemo katika maeneo ya Kapedo ambayo yamekuwa yakikumbwa na visa vya utovu wa usalama.
Zaidi ya watahiniwa milioni moja wanatazamiwa kukalia mtihani wa darasa la nane KCPE kuanzia Jumaattu wiki ijayo.
Watahiniwa 752,981 wanakalia mtihani wa kidato cha nne KCSE.