Kenya yaandikisha maambukizi mapya 1,064 ya corona

0

Kwa mara ya kwanza tangu wingu la tatu la corona kuripotiwa nchini, Kenya imerekodi idadi kubwa ya maambukizi mapya sawa na maafa ya ugonjwa huo.

Wizara ya afya imedhibitisha maambukizi mapya 1,064 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita baada ya kupima sampuli 6,151 na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 115,031.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema kuwa watu 165 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi hiyo kuwa 88,781.

Wagonjwa 7 zaidi wamefariki kutokana na ugonjwa huo na kufikisha idadi ya maafa nchini kuwa 1,925.

Wagonjwa 104 wamelezwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi (ICU).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here