Serikali yatetea kuongeza bei za mafuta

0

Huku vilio vya Wakenya vikiendelea kusikika kutoka sehemu mbalimbali nchini kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha, serikali imetetea hatua ya kuongezeka bei za mafuta.

Msemaji wa serikali kanali mstaafu Cyrus Oguna akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari anasema serikali haina lingine ila kuongeza ushuru ili ipate pesa za kuwahudumia wananchi wake.

Amesema ni jukumu la Wakenya kuisaidia serikali kutekeleza majukumu yake ipasavyo kupitia kulipa ushuru.

Oguna vile vile ametoa hakikisho kwamba imeweka mikakati makhususi kuhakikisha kwamba mitihani ya kitaifa inaendelea kote nchini pasipo kutatizika.

Amesema kila kitu kii shwari kabla ya kuanza kwa mitihani hiyo ikiwemo katika maeneo ya Kapedo ambayo yamekuwa yakikumbwa na visa vya utovu wa usalama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here