Sahihi za BBI zaendelea kutafutwa katika maeneo mbalimbali nchini

0

Shughuli ya kukusanya sahihi za mswada wa BBI imeendelea hii leo huku viongozi mbalimbali wakiongoza hafla hiyo katika maeneo tofauti nchini.

Gavana wa Nakuru Lee Kinyanjui ameongoza shughuli hiyo katika kaunti hiyo huku akiwarai Wakenya kuunga mkono mswada huo utakaoishia katika marekebisho ya katiba mwaka ujao.

Naye

Seneta wa Baringo Gideon Moi amepeleka shughuli ya kukusanya sahihi hizo katika kaunti ya Migori hii leo.

Mwenyekiti huyo wa chama cha KANU kwa mara nyingine amepigia debe mswada huo akisema una mengi yanayolenga kuwafaidi Wakenya.

Haya yanajiri siku moja baada ya Moi kuongoza shughuli kama hiyo katika kaunti ya Narok.

Hayo yakijiri

Katibu mkuu wa muungano wa vya wafanyikazi nchini COTU Francis Atwoli amewataka wasiokubaliana na mswada wa BBI kuanzisha kampeini ya kuipinga.

Atwoli akizungumza katika kaunti ya Kisumu amepigia debe mswada huo akisema utakuwa wa manufaa kwa taifa hili katika kuwezesha rasilimali zinafika mashinani.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here