Mahakama yazuia kushtakiwa kwa Matiang’i kuhusu ardhi ya Ruaraka

0

Mahakama ya Milimani imezima jitihada za mwanablogu Dennis Itumbi aliyetaka kumushtaki waziri wa usalama wa ndani Dkt. Fred Matiang’i kuhusiana na sakata ya ardhi ya Ruaraka.

Akitoa uamuzi huo, hakimu wa mahakama ya kupambana na ufisadi Douglas Ogoti ameelezea kuwa Itumbi alishindwa kuifahamisha mahakama namna alivyopata stakabadhi alizokuwa anapanga kutumia kumushtaki Matiang’i.

Itumbi ambaye hajaridhishwa na uamuzi huo amesema atakata rufaa katika mahakama ya kuu.

Itumbi anataka Matiang’I, wakati huo akiwa waziri wa Elimu, kushtakiwa kwa makosa manne ya ufisadi yanayohusiana na sakata ya ardhi hiyo ambapo shule ya msingi ya Drive Inn na ile ya upili ya Ruaraka zimejengwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here