Mahakama yaruhusu kuzikwa kwa Murunga

0

Mahakama imeruhusu kuzikwa kwa aliyekuwa mbunge wa Matungu Justus Murunga.

Uamuzi huu umetolewa na hakimu mkaazi Peter Muholi ambaye pia ameruhusu kuchukuliwa kwa sampuli za chembe chembe za DNA kutoka kwa mwili wa marehemu.

Hakimu Muholi ameridhia ombi hilo lililowasilishwa mahakamani na Agnes Wangui, mwanamke anayedai kuzaa watoto wawili na marehemu.

Hii inamaanisha kuwa mwili wa marehemu utaachiliwa ili kuzikwa wikendi hii au tarehe nyingine huku Wangui na wanawe wakiruhusiwa kushiriki kikamilifu kwenye mazishi ya mwenda zake.

Wangui aliambia mahakama kwamba marehemu Murunga alikuwa amemnunualia shamba huko Karen na alikuwa anapanga kumjengea nyumba ili waanze kuishi kama mtu na mkewe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here