Umma wapewa nafasi kutoa maoni kuhusu Sonko

0

Umma wana hadi Jumatano wiki ijayo kuwasilisha maoni yao kuhusu hoja ya kumbandua Gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko.

Jumla ya wawakilishi wadi 86 kati ya 122 wametia sahihi zao kwenye mswada huo wa kumuondoa na hivyo kupitisha idadi inayohitajika.

Mswada huo umewasilishwa bungeni na kiongozi wa walio wachache Michael Ogada.

Hata hivyo wawakilishi wadi wanaomuunga mkono gavana Sonko wametaja kuwa njama ya kumbandua imesababishwa na hatua yake kukataa kutia saini na kuidhinisha bajeti inayogharimu Sh37.5b ya mwaka 2020-2021.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here