Naibu Rais William Ruto kwa mara nyingine anawataka wanasiasa kukoma kueneza kile anasema ni siasa za ukabila.
Akizungumza alipoongoza hafla ya harambee kwa wahudumu wa boda boda katika uwanja wa Sironga kaunti ya Nyamira, Ruto amesema baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakitumia vijana kueneza siasa za migawanyiko.
Ruto ameongoza baadhi ya wanasiasa waliohudhuria mkutano huo kukahsifu kile wanasena ni baadhi ya maafisa wa ngazi za juu serikalini kutumia maafisa wa polisi kuwahangaisha.
Ruto amesema kuwa wanatafuta namna ya kuwasaidia wakenya wenye biashara ndogo ndogo nchini na kutaka kazi zao kuheshimiwa.









