Mkewe rais awashauri akina mama kupimwa Saratani ya matiti

0

Mkewe rais Margaret Kenyatta anawashauri akina mama kupimwa mapema kubaini hali yao ya saratani ya matiti.

Bi. Kenyatta anasema iwapo utapimwa mapema na kugundua kuwa unaugua ugonjwa huo, basi hii itawezesha matibabu ya haraka na kuokoa maisha.

Mkewe rais amesema haya katika ujumbe wake mwezi huu wa Octoba ambapo hamasisho dhidi ya ugonjwa huo wa saratani ya matiti linalotolewa.

Bi. Kenyatta vile vile amewapongeza akina mama mashujaa ambao walipambana na ugonjwa huo na kuushinda huku akiwatia moyo waliopatikana nao kuwa hali yao itaimarila.

Wakati uo

Kituo cha kupima na kutibu saratani kimefunguliwa rasmi katika kaunti ya Makueni.

Gavana Kivutha Kibwana ameongoza ufunguzi wa kituo hicho katika hospitali ya rufaa ya Makueni ambapo amewahimiza wenyeji kupimwa ili kugundua mapema iwapo wana ugonjwa huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here