Waliokuwa makamishna wa IEBC wateuliwa kuwa mabalozi

0

Waliokuwa makamishna wa tume ya uchaguzi na mipaka (IEBC) Consolata Maina Nkatha na Margaret Mwachanya wameteuliwa na rais Uhuru Kenyatta kuwa manaibu mabalozi.

Nkatha anapendekezwa kuwa balozi wa Kenya huko Roma nchini Italia huku mwenzake Mwachanya akitumwa Islamad.

Makamishna hao wawili walijiuzulu katika tume ya IEBC mwaka 2018 kwa misingi kwamba hawakuwa na imani na uongozi wa mwenyekiti Wafula Chebukati.

Balozi Martin Kimani ambaye ni katibu mwenza wa kamati ya BBI ameteuliwa kuwa mumbe wa Kenya katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) yenye makao yake mjini New York, Marekani.

Wengine walioteuliwa na rais kuwa mabalozi ni balozi John Tipis (Canberra), Immaculate Wambua (Ottawa) na balozi Catherine Mwangi (Pretoria). Jean Kamau anapendekezwa kuwa balozi mjini Addis Ababa, Linday Kiptiness (Bangkok), balozi Tom Amolo (Berlin), Lemarron Kaanto (Brasilia), balozi Daniel Wambura (Bujumbura) na Stella Munyi (Harare).

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here