Ruto awaongoza wendani wake kukashifu ufufuzi wa kesi za ghasia za baada ya uchaguzi

0

Naibu wa rais William Ruto amewaongoza wendani wake kukashifu vikali  hatua ya kufufuliwa kwa kesi  za baada ya uchaguzi  wa mwaka 2007/08.

Kupitia mtandao wake wa Twitter, Ruto amesema hatua hiyo ni njama ya kurejesha ukabila na kuzuia juhudi za mrengo wake wa husler kukabili umaskini kwa kuhakikisha vijana wanapata mbinu za kufanya biashara imetokomeza ukabila.

Naye

Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi ameelezea kutamaushwa kwake na hatua hiyo akisema itasababisha uhasama wa kikabila baada ya rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kushirikiana kisiasa kabla ya uchaguzi wa mwaka 2013.

Mbunge huyo amedai huyo idara ya DCI inatumika kuafikia malengo ya kisiasa.

Sudi vile vile amewatahadharisha Wakenya dhidi ya kukubali kugawanywa kwa misingi ya kikabila kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022.

Kauli za Sudi zimetiliwa mkazo na zaidi  ya wabunge 40 na viongozi wa bonde la ufa wanaomunga mkono Ruto wamemkosoa DCI wakisema kuwa hatua ya kufufua kesi hizo itaibua uhasama baina ya wakenya.

Katika kauli ambayo imesisitizwa na senata wa Nakuru Susan Kihika na mwenzake wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen, viongozi hao wanasema kuwa wakenya wamesameheana.

Wakati uo huo

Aliyekuwa mbunge wa Kibwezi Kalembe Ndile ameunga mkono kuchunguzwa upya kwa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2007/08.

Ndile amesema hatua hiyo itahakikisha kuwa walioathirika na ghasia hizo  wamepata haki.

Akizungumza mjini Machakos, Kalembe ameeleza kuwa hii ndio njia pekee ya kuwafikia maskini waliodhulumiwa wakati wa ghasia hizo iwapo wahusika watahukumiwa.

Na huku kauli hizo zikiendelea kutolewa

Idara ya upelelezi nchini DCI sasa inasema haifufui tena kesi zinazohusiana na machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu wa 2007/08.

Badala yake mkurugenzi wa idara hiyo George Kinoti amesema uchunguzi walioanzisha unahusiana na lalama kutoka kwa baadhi ya waathiriwa waliodai kutishiwa maisha.

Amesema kusudi lao sio kufungua upya faili za kesi zilizokamilika ila ni kuchunguza kesi dhidi ya watuhumiwa waliokwepa mkono wa sheria.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here