Shughuli ya kusanya sahihi za BBI kuzinduliwa Jumatano

0

Shughuli ya kukusanya sahihi za kufanyia katiba marekebisho kupitia mchakato wa BBI itazinduliwa Jumatano wiki hii ambayo ni Novemba 25.

Mwenyekiti wa kamati inayoongoza shughuli hiyo Dennis Waweru anasema rais Uhuru Kenyatta pamoja na ndugu yake kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga wanatazamiwa kuongoza uzinduzi huo.

Uzinduzi huo ulihairishwa kufuatia kucheleweshwa kuchapishwa kwa mswada marekebisho ya katiba.

Odinga Jumatatu alikutana na viongozi kutoka eneo la Mlima Kenya wakiongozwa na aliyekuwa mbunge wa Gatanga na muwaniaji wa urais Peter Kenneth kutafuta ushawishi wa kuungwa mkono kwa ripoti hiyo.

Haya yanajiri licha ya ripoti hiyo kuendelea kupokea pingamizi kutoka kwa wadau mbalimbali wa hivi punde wakiwa ni viongozi wa Kiislamu chini ya muungano wa SUPKEM.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here