Mahakama ya Nairobi imeagiza kushikwa kwa mbunge wa Kimilili Didmus Barasa na afungwe miezi sita kwa kushindwa kulipa deni.
Hakimu DM Kivuti ameagiza waranti ya kukamatwa kwa mbunge huyo kupewa OCS wa kituo cha Polisi cha Central.
Barasa alikuwa na hadi Jumanne kumlipa wakili wake Alfred Ndambiri deni la Sh1.8M lakini akahepa kufanya hivyo wala kufika mahakamani.
Wakili huyo amekuwa akimdai mbunge huyo deni hilo baada ya kumwakilisha kesi iliyowasilishwa mahakamani na aliyekuwa mbunge Suleiman Murunga kupinga uchaguzi wake.
Wawili hao wamekuwa wakidaiana deni hilo kuanzia wakati huo ndiposa wakili huyo akaamua kumushtaki mbunge huyo.