IEBC yatoa mfumo utakaotumika kusanya sahihi za BBI

0

Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imetoa mfumo utakaotumika katika kukusanya sahihi za kubadilisha katiba kupitia mchakato wa BBI.

Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati ametoa mwongozo huo baada ya kamati ya BBI kutuma ombi la kutaka kuelezwa aina ya sahihi zinazohitajika.

Wakati uo huo kundi moja la wanawake limepinga ripoti ya BBI likihoji kuwa itarudisha nyuma hatua zilizopigwa katika kuwapa wanawake nafasi sawa kwenye nyadhifa za uongozi.

Kundi hilo likiongozwa na Daisy Amdanyi, Dorothy Otieno na Jerotich Seii limeapa kuwashawishi wenzao kupinga ripoti hiyo kwa misingi kwamba haijatoa mwongozo kuhusu ni vipi wanawake wanafaidika.

Kauli zao zinajiri siku moja kabla ya rais Uhuru Kenyatta na ndugu yake Raila Odinga kuzindua shughuli ya kukusanya sahihi za kufanyia katiba marekebisho kupitia BBI baada ya kuhairishwa mara ya kwanza.

Yakiarifia hayo

Mabunge ya kaunti za Kericho na Nandi yameelekea katika mahakama ya upeo kutafuta ushauri kuhusina na mswada wa marakebisho ya katiba mwaka 2020 kupitia kwa ripoti ya BBI.

Mabunge hayo yanataka kufahamu, miongoni mwa masuala mengine, idadi ya waakilishi wadi ambao wanahitajika kupitisha mswada huo.

Mabunge hayo pia yanataka kufahamu iwapo yanaweza kupendekeza marekebisho kwneye mswada huo baada ya kufanya vikao vya umma.

Mabunge ya kaunti 47 nchini ni muhimu kwani angalau 24 ni sharti yapitishe mswada huo wa marekbisho ya katiba kabla ya kura ya maamuzi kufanyika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here