Ruto apeleka kampeini za kuwania urais Kilifi

0

Naibu Rais William Ruto amejitetea kuhusiana na madai kuwa ahadi anazotoa kwa wakenya ni hewa na kwamba hazitimizwi.

Akizungumza katika kaunti ya Kilifi, Ruto amesema serikali ya Jubilee imetekeleza ahadi ilizotoa kwa wakenya ikiwemo ujenzi wa miundo msingi na pia kuunganishia umeme kwa zaidi ya makaazi million 25.

Ruto ametetea siasa zake za hasla na kusema zinalenga kuwainua watu wa chini huku akikashifu wale wanaounga mkono BBI akidai kuwa wanajitafutia makuu.

Ruto amezindua ujenzi wa barabara ya Kilifi-Bamba na kusema mwanakandarasi ataanza kazi hivi karibuni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here