Raia wa Marekani anayetuhumiwa kuwabaka wasichana wadogo katika makaazi yake ya watoto kaunti ya Bomet amefungwa zaidi ya miaka 15.
Gregory Dow mwenye umri wa miaka 61, amepewa kifungo hicho na Mahakama ya Pennsylvania nchini Marekani baada ya kupatikana na hatia ya kuwanajisi wasichana wanne wenye umri wa kati ya miaka kumi na moja na kumi na tatu kati ya mwaka 2013-2017.
Katika uamuzi wake, mahakama imesema kuna ushahidi wa kutosha kudhibitisha kuwa mshukiwa aliwabaka watoto hao ambao alifaa kuwapa ulinzi.
Makaazi hayo ya watoto katika eneo la Boito yalifungwa na serikali mwaka 2017 na mshukiwa akatoroka nchini kabla ya kukamtwa ili afunguliwe mashtaka.









