Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amesema oparesheni ya kijeshi katika eneo la Kapedo itaendelea hadi wanaohusika na visa vya utovu wa usalama washikwe.
Odinga akizungumza baada ya kupeleka kampeini za BBI Turkana amesema amani itarajea katika maeneo hayo kufuatia oparesheni hiyo ya kiusalama.
Waziri huyo mkuu wa zamani vile vile amepigia debe BBI akisema itatoa suluhu kwa matatizo mengi ambayo yamekuwa yakilihangaisha taifa hili.