Naibu rais William Ruto sasa anaitaka serikali kuacha kukopa madeni mengi yanayowafinya Wakenya.
Akizungumza huko Elgeyo Marakwet, Ruto anasema kiu cha serikali kukopa madeni kutoka Uchina kimeendelea kusambaratisha uchumi wa taifa la Kenya huku mwananchi wa kawaida akiumia.
Ruto vile vile amepigia debe siasa zake za walala hai na walala hoi akisema yeye hatasubiri kuungwa mkono na yeyote.