Kenya imerekodi visa vipya 208 vya ugonjwa wa corona baada ya kupima sampuli 3,415 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.
Waziri wa afya Mutahi Kagwe anasema hii inafikisha 104,201 idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini kufikia sasa.
Idadi ya waliopona imefikia 85,577 baada ya kupona kwa watu wengine 37 huku waliofariki wakifikia 1,823 baada ya kufariki kwa wagonjwa 6 zaidi.
Wagonjwa 51 wako katika chumba cha watu mahututi, 24 wakisaidiwa na mashine kupumua.