Rais Ruto Aagiza Shilingi Milioni 5 kwa Taasisi Zilizoshiriki Tamasha la Muziki.

0

Rais William Ruto ameiagiza Wizara ya Elimu kutoa shilingi milioni 5 kwa kila shule na taasisi iliyoshiriki katika Tamasha la Kitaifa la Muziki 2026, kwa lengo la kukuza sanaa na ubunifu.

Akizungumza Ijumaa tarehe 14 Agosti wakati wa tamasha la 98 la Muziki wa Shule za Kenya, Rais Ruto alimwagiza Waziri wa Elimu Julius Migos Ogamba kuanza maandalizi ya kutolewa kwa fedha hizo, ambazo zitatumika kuboresha miundombinu na vifaa vya shughuli za muziki na ubunifu.

“Kuna zaidi ya shule 30 zimeshiriki katika tamasha hii leo. Ninaiomba Wizara ya Elimu kutoa shilingi milioni tano kwa kila shule na taasisi kama ishara ya shukrani na kutambua ushiriki wao.”

Rais amesema fedha hizo pia zitasaidia shule hizo kujiandaa vyema kwa mashindano ya muziki ya mwaka ujao 2027.

Aidha, Rais Ruto alitangaza mipango ya kupanua mradi unaopendekezwa wa Smart City mjini Bungoma, akiiagiza Wizara ya Ardhi kuufanyia marekebisho ili uweze kuhudumia wakazi wengi zaidi.

Tangazo hilo lilitolewa wakati shule mbalimbali zikitambuliwa kwa kufanya vizuri katika Tamasha la 98 la Muziki wa Shule za Kenya.

Shule ya Moi Forces Academy iliyoko jijini Nairobi iliibuka mshindi katika kitengo cha shule za chekechea, huku Aga Khan Academy Mombasa ikiongoza katika kitengo cha shule za msingi.

Shule ya Upili ya Wasichana ya Bunyore ilitajwa kuwa shule bora ya upili, huku Chuo kikuu cha Kenyatta kikishinda katika kitengo cha vyuo vikuu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here