Upo uwezekano kwamba rais Uhuru Kenyatta atakaza kamba kwenye masharti ya kuzuia msambao wa virusi vya corona atakapolihutubia taifa leo.
Rais anatarajiwa kupiga marufuku mikutano ya kisiasa, kuongeza muda wa kafyuu inayoanza saa nne usiku huku ikiarifiwa kwamba huenda akafunga tena maeneo ya burudani kufuatia kuongezeka kwa msambao wa virusi hivyo.
Katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita, watu 829 wamepatikana na virusi hivyo kati ya sampuli 6,239 zilizopimwa na kufikisha idadi ya jumla ya maambukizi nchini kuwa 111,185.
Waziri wa afya Mutahi Kagwe amedhibitisha kupona kwa watu wengine 91 na kufikisha idadi hiyo kuwa 87,994.
Aidha mtu mmoja amefariki kutokana na makali ya virusi hivyo na kufikisha idadi ya maafa kuwa 1,899.