Haki Afrika wataka uchaguzi mkuu wa 2022 uhairishwe

0

Shirika la Haki Afrika linapendekeza kuhairishwa kwa uchaguzi mkuu wa 2022 kutokana na janga la COVID19.

Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Hussein Khalid anahoji kwamba uchaguzi huo unafaa kuhairishwa kwa sababu mikutano ya kisiasa imekuwa ndio chanzo kikuu cha kusambaa kwa virusi vya corona.

Haki Afrika vile vile limeunga mkono kupigwa marufuku kwa mikutano yote ya kisiasa ili kuzuia msambao wa virusi hivyo.

Kauli hizi zinajiri wakati ambapo kinara wa chama cha ODM amejiweka kwenye karantini baada ya kukutwa na ugonjwa wa corona.

Odinga katika taarifa amedhibitisha kuwa amekutwa na ugonjwa huo baada ya kupimwa zaidi ya mara moja na sasa yuko kwenye karantini kulingana na taratibu za wizara ya afya.

Waziri huyo mkuu wa zamani amepatwa na corona siku chache baada ya kuongoza misururu ya kupigia debe mswada wa marekebisho ya katiba BBI katika eneo la Pwani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here