Waliopata D+ hawatajiunga na Polisi asema Matiang’i

0

Idara ya Polisi hivi karibuni itaacha kuwasajili makurutu waliopata gredi ya D+ kujiunga nayo kama njia mojawapo ya kuimarisha vita dhidi ya uhalifu.

Waziri wa usalama wa ndani Dkt. Fred Matiang’i anahoji kuwa idara hiyo inakabiliwa na changamoto kufanikisha kushtakiwa kwa washukiwa wa uhalifu kwa sababu masomo ya baadhi ya maafisa wa Polisi ni ya china mno hali inayofanya vigumu kutekeleza majukumu yao vilivyo.

Akizungumza kwenye hafla ya kufuzu kwa maafisa wapya katika afisi ya mwendesha mkuu wa mashtaka ya umma, waziri wa usalama wa ndani Dkt. Fred Matiang’i amesema ushirikiano wa karibu pekee baina ya asasi husika ndio utafanikisha kikamilifu vita dhidi ya uhalifu.

Afisa mkuu mtendaji wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi (EACC) Twalib Mbarak amewatahadharisha maafisa hao dhidi ya kuchukua hongo.

Kwa upande wake mwendesha mkuu wa mashtaka ya umma Noordin Hajji amewasihi wafanyikazi hao waliopata mafunzo makhususi kuwajibikia majukumu yao kwa kuzingatia maadili mema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here