Rais Kenyatta avunja kimya kuhusu mswada tata wa ugavi wa mapato

0

Kamati ya watu 12 iliyoteuliwa kutanzua mgogoro unaozingira mswada tata wa ugavi wa mapato imekutana na maafisa kutoka wizara ya fedha sawa na mamlaka ya mapato nchini CRA kutafuta mwafaka kuhusu utata huo.

Haya yanajiri huku rais Uhuru Kenyatta akivunja kimya chake kuhusiana na mswada huo.

Akizungumza wakati wa kutoa vyeti kwa wakaazi wa Embakasi katika jumba la mikutano la KICC, rais Kenyatta amekanusha madai ya kuingilia mjadala huo na kusisitiza kuwa mamlaka ya mapato nchini CRA ndio ilipendekeza mfumo unaofaa kutumika kugawa pesa kwenye serikali za kaunti.

Rais Kenyatta vile vile amesema lengo la kuu ni kuwahudumia Wakenya na wala sio kujihusisha na siasa zisizokuwa na msingi.

Naye naibu rais William Ruto ametoa changamoto kwa bunge la Senate kuhakikisha kuwa mfumo utakoafikiwa kugawa rasilimali za kitaifa katika serikali za kaunti ni wa usawa.

Ruto amesema kaunti zenye watu wengi ziongezewe mgao zaidi ila kaunti zenye watu wachache zisinyanganywe kidogo walicho nacho.

Matamshi ya rais na naibu wake yanawadia huku kamati ya maseneta kumi na wawili iliyobuniwa kutanzua mgogoro huo ikitazamiwa kuwasilisha bungeni ripoti yake Jumatatu wiki ijayo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here