ODM ‘inawatetea wafisadi’

0

Chama cha ODM kimejipata mashakani baada ya taarifa yake kuhusiana na madai ya wizi wa pesa katika shirika la KEMSA kuonekana kuwakinga wezi.

Naibu Rais William Ruto ameongoza viongozi wengine kukahsifu taarifa hiyo iliyotolewa na katibu mkuu wa ODM Edwin Sifuna na kusema huenda mkataba wao na Rais Uhuru Kenyatta ulilenga kuwapa nafasi ya kuiba mali ya umma.

Baadhi ya viongozi wa kisiasa wakiwemo wabunge Caleb Kostany na Ndindi Nyoro sasa wanakitaka chama cha ODM kujitokeza wazi kusema kile wanajua kuhusiana na sakata hiyo.

Nao muungano wa wauguzi nchini KNUN kupitia kwa katibu wake mkuu Seth Panyako unasema matamshi ya Sifuna yanatamausha.

Viongozi wa kidini nao hawajaachwa nyuma, wakiongozwa na Askofu Mark Kariuki, viongozi hao wamelaani vikali wizi wa mali ya umma na wanaitaka serikali kuzidisha juhudi za kutokomeza uozo huo nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here