Watu 16 zaidi wamefariki kutokana na ugonjwa wa corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya maafa kuwa 532.
Katibu katika wizara ya afya Dkt. Mercy Mwangangi amesema idadi ya waliopona kutokana na ugonjwa huo imeongezeka na kufikia 18,157 baada ya kupona kwa watu 288 zaidi.
Idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini imeongezeka na kufikia 31,763 baada ya visa vipya 322 kudhibitishwa.
Msambao wa visa hivyo ni kama ifwatavyo; Nairobi 106, Kajiado 53, Machakos 25, Nakuru 25, Kiambu & Kisii 23, Busia 13, Mombasa 11, Kisumu & Bomet 5, Garissa, Homabay & Nandi 4, Uasin Gushu, Kitui, Nyandarua, Taita Taveta , Turkana 3 na Nyamira 2.
Wakati uo huo, wizara hiyo imesema wahudumu wa afya 885 wameambukizwa virusi hivyo vya corona huku 16 kati yao wakifariki.