ODM waafikia kushirikiana na Jubilee kuunga mkono BBI

0

Kamati kuu ya chama cha ODM chini ya uongozi wake kinara Raila Odinga imeafikia kuungana na chama tawala cha Jubilee kupigia debe mswada wa marekebisho ya katiba BBI.

Katika taarifa naibu katibu mkuu wa chama hicho Agnes Zani amesema kuwa nia yao ni kuona taifa lenye umoja.

Wanaotaka kuwania urais kwa tiketi ya chama hicho mwaka 2022 wanafaa kutuma maombi yao kufikia tarehe 26 mwezi huu.

Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya na mwenzake a Mombasa Ali Hassan joho tayari wameelezea nia yao ya kumenyana na kinara wa chama hicho Raila Odinga kupata tiketi ya Chungwa kuelekea ikulu.

Hayo yakijiri

Wakilishi wadi wa kaunti ya Baringo wanaoegemea mrengo wa naibu rais William Ruto wamepinga madai kuwa mchakato wa kujadili mswada wa BBI haukufuata sheria.

Wakiongozwa na mwakilishi wadi wa Mochongoi Kipruto Kimosop, MCAs hao wanasema spika David Kiplagat alitoa uamuzi kuhusu mswada huo ikiwemo kutangaza matokeo ambapo kwa mujibu wao, mswada huo uliangushwa na waakilishi wadi 30.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here