Chama cha Amani National Congress (ANC) sasa kinadai kuwa wenzao wa ODM hawaruhusiwi kuwa na mgombea wa urais kwenye uchaguzi mkuu wa 2022.
Chama hicho kinachoongozwa na Musalia Mudavadi kinadai kuwa makubaliano ya muungano wa NASA yangalipo kwa sababu kufikia sasa hakuna aliyejiondoa rasmi kwenye muungano huo.
Kauli hizi zinajiri wakati ambapo chama cha ODM kinajiandaa kwa uchaguzi mkuu wa 2022 kwa kuitisha maombi kwa wanaotaka kuwania urais kwa tiketi ya chama hicho sawa na kujiandaa kwa chaguzi za mashinani hivi karibuni.
Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya na mwenzake a Mombasa Ali Hassan joho tayari wameelezea nia yao ya kumenyana na kinara wa chama hicho Raila Odinga kupata tiketi ya Chungwa kuelekea Ikulu.