Kenya haijaripoti maafa yoyote yanayotokana na ugonjwa wa corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na hivyo idadi hiyo inasalia kuwa 1,794.
Waziri wa afya Mutahi Kagwe amedhibitisha kupatikana kwa maambukizi mapya 260 baada ya kupima sampuli 5,873 na kufikisha idadi ya visa hivyo kuwa 102,613.
Watu 83 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 84.873.
Idadi ya wagonjwa waliolazwa hospitalini ni 341 na watu 1,319 wanashughulikiwa nyumbani.
Watu 30 wako katika chumba cha watu mahututi.
Msambao katika kaunti ni kama ifuatvyo Nairobi 131, Baringo 50, Uasin Gishu 10, Machakos 9.