Msiruhusu wanasiasa kutumia makanisa visivyo, viongozi wa kidini wahimizwa

0

Waziri wa usalama wa ndani Dkt. Fred Matiang’i ameyataka makanisa yasiruhusu majukwaa yao kutumika na wanasiasa kuwagawanya watu.

 Dkt. Matiang’i vile vile amewasihi viongozi wa kidini kutojihusisha na siasa za migawanyiko wakati huu ambapo joto la kisiasa linazidi kupanda nchini.

Waziri wa usalama amesema haya alipohudhuria ibada katika kanisa Katoliki dayosisi ya Murang’a.

Mawaziri Mutahi Kagwe (Afya) na mwenzake wa Uchukuzi James Macharia pamoja na katibu katika wizara ya elimu Zack Kinuthia walihudhuria ibada hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here