Naibu rais William Ruto kwa mara nyingine amewakanya wanasiasa wenzake dhidi ya kuendeleza siasa za ukabila.
Akizungumza alipoongoza uchangishaji wa pesa kuwasaidia wana bodaboda katika uwanja wa Kawaida eneo la Kiamba kaunti ya Nyeri, Ruto amesema umoja wa taifa hili ni muhimu kuliko jambo lolote.
Naibu rais vile vile amewasuta vikali watu anaosema wanawatumia vijana kuzua vurugu kwenye mikutano yake ya kisiasa.