Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amemsuta naibu rais William Ruto kutokana na kile ametaja kama kuwahadaa Wakenya.
Odinga akizungumza alipokutana na baadhi ya vijana kutoka kaunti ya Nairobi amesema Ruto ameendelea kutoa ahadi za uongo kwa Wakenya ilhali ahadi walizotoa kipindi cha uchaguzi bado hazijatekelezwa.
Waziri huyo mkuu wa zamani vile vile amepinga wazo la kutaka uchaguzi mkuu wa mwaka ujao kuandaliwa sambamba na kura ya maamuzi akisema wapiga kura watachanganyikiwa.