Dereva aponea baada ya trela kutumbukia baharini Likoni

0

Dereva mmoja ameponea baada ya trela aliyokuwa akiendesha kuanguka baharini katika kivuko cha Likoni kaunti ya Mombasa.

Shirika la feri nchini limedhibitisha ajali hiyo iliyotokera saa kumi na robo alfajiri baada ya dereva kupoteza mwelekeo alipokuwa anaingiza trela hiyo ndani ya feri.

Kisa hicho kilisababisha msongamano mkubwa katika kivuko hicho ambacho kinategemewa na wakaazi wanaoenda kazini.

Hadi tukienda mitamboni, shughuli za uokozi zilikuwa zinaendelea kujaribu kutoa trela hiyo ndani ya bahari.

Inaripotiwa kuwa trela hiyo ilikuwa imebeba mahindi kutoka Tanzania ikielekea mjini Mombasa kabla ya ajali hiyo kutokea.

Ajali hii inajiri siku tatu tu baada ya gari nyingine kutumbukia baharini katika kivuko hicho baada ya dereva wake pia kupoteza mwelekeo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here